Ligi ya Taifa Ngazi ya Mkoa wa Iringa Iliendelea hapo jana kwa kuwakutanisha timu ya AL-JAZEERA F.C kutoka Ruaha Mbuyuni Wilayani Kilolo na vinara wa kundi B timu ya SENGO F.C ya Mjini Iringa; pambano hilo kumalizika kwa Timu ya SENGO F.C kuibugiza bila huruma timu ya AL-JAZEERA kwa mabao 3 - 0.
Mchezo huo uliofanyika katika Dimba la Samora mkoani Iringa, ilishuhudia timu ya SENGO F.C ikitandaza soka safi na lakuvutia na kujipatia bao la mapema dakika ya 7 ya mchezo likiwekwa kimiani na kiungo machachari MESHACK MALINGA baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la AL-JAZEERA F.C. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika SENGO F.C walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa kwa vijana wa AL-JAZEERA F.C wakitaka kusawazisha na kuondoa uteja kwenye ligi hiyo, ila hali ilikuwa tete baada ya SENGO F.C kufanya mabadiliko ya kuwatoa STEVE MATHEW na MESHACK MALINGA na nafasi zao kuchukuliwa na KILONGE MYINGA na FRED GEORGE; mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwa timu ya SENGO F.C kujipatia mabao mawili zaidi kupitia kwa CHESCO MAKWETA na KILONGE MYINGA. Hadi mwisho wa mchezo SENGO F.C iliibuka na ushindi huo mnono unaowaweka kwenye nafasi nzuri ya kuongoza kundi lao la B na kujipatia nafasi ya kucheza hatua ya TATU BORA.
SENGO F.C iliwakilisha na 1. ABDALLAH MAKANGANA/MICHAEL LIDUKE 2. KIMILIKE 3. DANIFORD KIGODI "KIMTI" 4. JULIUS MWAKENJA 5. NKANO JOSEPH 6. SHABAN JAIRO 7. MESHACK MALINGA/FREDY GEORGE 8. ALEX MBEWE 9. CHESCO MAKWETA 10. STEVE MATHEW/KILONGE MYINGA 11. ELIAH NYONDO

No comments:
Post a Comment