Wawakilishi
wa Tanzania bara kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu
ya Young Africans leo imeanza vizuri mashindano hayo kwa kuibuka na
ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni kutoka visiwa
vya Comoro katika mchezo uliofanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.
Ikicheza mbele ya mashabki wake takribani elfu 17 katika Uwanja wa
Taifa, kikosi cha Young Africans kiliweza kucheza vizuri na kutumia
nafasi hizo ambapo imeweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga
mbele katika hatua inayofuata kutokana na kuhitaji droo tu ya aina
yoyote.
Mrisho Ngasa aliwainua mashabiki wa Young Africans vitini
dakika ya 13 ya mchezo kufuatia kuukwamisha mpira wavuni kwa kichwa
baada ya pasi ya iliyopigwa na mlinzi wa kulia Mbuyu Twite kumkuta
mfungaji na kuumwamisha mpira wavuni bila makosa.
Dakika
ya 20 ya mchezo, nahodha wa Young Africans Nadir Haroub "Cannavaro"
aliipatia Young Africans bao la pili kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu
uliopigwa na David Luhende kuunganisha moja kwa moja wavuni.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 2 - 0 Komorozine de Domoni.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Didier
Kavumbagu aliiingia kuchukua nafasi ya David Luhende.
Dakika
ya 58 Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao la tatu baada ya
kumalizia pasi safi ya Mrisho Ngasa aliyewatoka walinzi wa Komorozine de
Domoni upande wa kulia na kumpasia Kavumbagu ambaye aliukwamisha mpira
wavuni.
Hamis Kiiza "Diego" aliwainua mashabiki wa Young Africans
vitini dakika ya 59 ya mchezo kufuatia pasi ya Didier Kavumbagu
aliywatoka walinzi wa Komorozine de Domoni.
Mrisho
Ngasa aliipatia Young Africans bao la tano dakika ya 65 ikiwa ni dakika
moja baadae baada ya kazi nzuri iliyofanywa na na viungo wa Young
Africans Haruna Niyonzima na Frank Domayo.
Dakika tatu baadae
Mrisho Ngasa aliifungia Young Africans bao la sita na likiwa ni bao bao
lake la tatu katika mchezo wa leo baada ya kumalizia mpira wa Saimon
Msuva uliokoloewa na golikipa wa Komorozine.
Dakika ya 81 ya
mchezo, Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao saba kufuatia
kuitumia vizuri pasi ya mshambuliaji Hamis Kiiza ambapo Kavumbagu bila
ajizi alimchambua mlinda mlango wa timu ya Komorozine.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 7- 0 Komorozine de Domoni.
Mchezo
wa marudiano utafanyika wiki ijayo kati ya tarehe 14,15,16 Februari
Visiwa vya Comoro ambapo Young Africans inahitaji sare ya aina yoyote
ili kuweza kusonga mbele kutofungwa mabao zaidi ya 6-0 katika mchezo
huo.
Kocha wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema anshukuru
vijana wake wamecheza vizuri, wamepata nafasi za kufunga wamezitumia
japo sio zote, kikubwa tutaendelea na mazoezi kufanyia marekebisho
makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa leo.
Young Africans: 1.Juma
Kaseja 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro",
5.Kelvin Yondani/Rajab Zahir, 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Saimon
Msuva/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima, 9.Hamis Kiiza, 10.Mrisho
Ngasa, 11.David Luhende/Didier Kavumbagu

No comments:
Post a Comment