Sikio la kufa halisikii dawa ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya Klabu Bingwa Tanzania Bara imba Sport Club "Wekundu wa msimbazi" kukubali kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa Mtibwa Sugar ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba iliyofanikiwa kuifunga Prisons ya Mbeya kwa Goli moja wiki iliyopita ilikoa umakini na ubora wake katika mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar hali iliyopelekea hata baadhi ya mashabiki wake kuizomea muda mwingi wa Mchezo....
Kwa matokeo hayo Simba bado inaendelea kukamata nafasi ya tatu, huku Watani wake wa jadi wakiongoza ligi hiyo kwa pointi 36, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 33.
No comments:
Post a Comment