Yanga 1-0 Azam
Dar
es Salaam Young Africans wamezidi kujichmbia kileleni mwa Ligi Kuu
Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya
Azam. Bao pekee la Yanga lilifungwa na Haruna Niyonzima katika dakika ya
31 baada ya kupokea pasi safi toka kwa Jerryson Tegete. Yanga ambao
walicheza soka safi na ya kuvutia kipindi cha kwanza wangeweza kupata
mabao mengi kama Jerryson Tegete
angekuwa makini kwani alipoteza nafasi tatu za wazi. Kipindi cha pili
azam walikianza kwa kushambulia wakitafuta bao la kusawazisha lakini
golikipa Ally Mustapha Barthez alikuwa imara langoni kuzuia kashikashi
zote za John Bocco na Kipre Tchetche. Kwa matokeo hayo sasa Yanga
inajitanua kileleni ikiwa na pointi 39 baada ya michezo 17 huku Azam
ikibaki na zake 36.
No comments:
Post a Comment