Klabu ya soka ya SENGO F.C, leo imeihadhiri timu ya soka ya KILOLO STARS kwa kuichapa magoli 7-2 katika muendelezo wa ligi ya daraja la Tatu Mkoa wa Iringa hatua ya makundi; mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Samora katika Manispaa ya Iringa.
Ligi hiyo ambayo ilihairishwa mara kwa mara tangu mwaka jana Novemba 2012, hatimaye ilianza jana kwa kufanyika mchezo mmoja uliokutanisha miamba ya Changarawe F.C dhidi ya Tango F.C; kwa ushindi wa magoli 2 - 0 kwa CHANGARAWE F.C; Huku mchezo wa BBC F.C dhidi ya MTERA SHOOTING STARS ukishindwa kufanyika kufuatia timu ya MTERA SHOOTING STARS kushindwa kufika Uwanjani.
SENGO F.C moja ya timu inayotazamiwa kuchukua Ubingwa wa Mkoa wa Iringa, iliuanza mchezo huo taratibu hadi dakika ya 16 ilipobadilika na kuanza kuishushia mvua ya mabao timu ya KILOLO STARS, Hadi mapumziko SENGO F.C ilikuwa mbele kwa mabao 3-1; kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa KILOLO F.C baada ya kuzidiwa kabisa na kuruhusu kuongezwa mabao mengine 4 hivyo kufanya matokeo yawe 7-1 kabla ya kupata penati na kufungwa kiufundi; hivyo matokeo kuwa 7-2 kwa SENGO F.C.
LIGI HIYO ITAENDELEA TENA KESHO KWA MCHEZO KWA MCHEZO KATI YA SUNSHINE F.C DHIDI YA ISIMANI UNITED.
STEVEN MATHEW, CHESCO MAKWETA HITS HATRICKS WHILE DANFORD KIGODI SCORES
ReplyDelete