Klabu bingwa za Tanzania Bara na Visiwani, Simba SC na Jamhuri zimeshindwa kuliwakilisha vyema Taifa la Tanzania mara baada ya kukubali vipigo vikubwa kutoka kwa Recreitivo Libolo ya Angola na St. George ya Ethiopia.
Simba ambayo ilifungwa goli 1-0 jijini Dar es Salaam ilitakiwa kushinda mchezo huo kwa magoli zaidi ya mawili ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika; lakini hali ilikuwa tete mara baada ya kukubali kipigo cha Magoli 4-0 kutoka kwa Waangola hao; kwa matokeo hayo Simba imetolewa kwa jumla ya mabao 5-0.
Nayo Jamhuri ya Visiwani Zanzibar imekubali kipigo cha mabao 5-0; huku Azam ikiwatoa Wasudan Kusini kwa mabao 8-1, mara baada ya leo kupata ushindi wa mabao 5-0. Azam ndio timu pekee iliyosalia kwenye michuano mikubwa inayoandaliwa na CAF kutoka Tanzania.
No comments:
Post a Comment